Na Henrick Idawa,Makete
Wagombea wote wa Ubunge jimbo la Makete Mkoani Njombe wametangazwa kuwa ni wagombea halali na hata mmoja wao hajawekewa pingamizi baada ya muda wa mapingamizi kumalizika huku mapingamizi yakijitokeza kwa upande wa madiwani katika kata mbalimbali
Akizungumza na kituo hiki ofisini kwake Msimamizi msaidizi wa uchaguzi jimbo la Makete Fadhili Nkenza amesema wagombea hao wa ubunge kutoka vyama vinne wanatakiwa kuendelea na hatua zinazofuata kwa kuwa hawajawekewa pingamizi
“Hatujapokea pingamizi
hata moja hivyo wagombea wote w vyama vinne,Festo Richard Sanga wa CCM,Joma
Mwakisitu wa ACT wazalendo na Ahady Tweve wa Chadema pamoja na Grace Njekela wa
NCCR Mageuzi wote ni wagombea halali wa nafasi za ubunge kwa hiyo wataruhusiwa
na kampeni kwa mujibu wa ratiba zetu” Fadhili Nkenza Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi jimbo la Makete
“Kuna pingamizi kutoka
kata ya Lupila ambapo mgombea wa chama cha Mapinduzi amempinga mgombea wa
Chadema,kuna pingamizi pia kata Mbalanze hawa wote wamepingana wa Chadema
amepinga wa CCM na wa CCM amempinga wa Chadema,Kata ya Iwawa mgombea wa CCM amempinga
wa Chadema,kata ya Kipagalo wote walipingana na kata ya Luhumbu pia vyama
vitatu vya ACT,NCCR na CCM walipingana,Kata ya Lupalilo CCM walimpinga mgombea
wa Chadema lakini pia na kata zingine waliendelea kupingana”aliongeza Fadhili
Nkenza Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi
jimbo la Makete
0 Comments