TANGAZA NASI

header ads

Migogoro ndani ya CCM Njombe itamalizwa na CCM yenyewe


Na Gabriel Kilamlya,Njombe

Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kimesema Matatizo ya Kisiasa ya Ndani ya CCM Yatamalizwa na Wanaccm Wenyewe Kwani Hakuna Wakuingilia Mambo Yao ya Ndani.

Wakati wa Kufunga Zoezi la Uchukuaji Fomu Katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Kwa Wagombea Wao Sita wa Nafasi ya Ubunge Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole Amesema Kuwa Hakuna chama Cha Siasa Chenye  Watu Wengi Wenye  Akili Tofauti Tofauti na Wasipishane hasa Katika Kipindi Hiki Cha Uchaguzi Huku Akizungumzia Mgogoro wa Wagombea Udiwani Katika Kata ya Mjimwema Mjini Njombe kwamba Wanakwenda Kuumaliza.

"Tumehitimisha zoezi la kuchukua fomu kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo yetu yote sita yanayounda mkoa wa Njombe,tunauhakika wagombea wote katika mkoa wa Njombe,mwezi Octoba wanaenda kutangazwa kama Wabunge wanaounda mkoa wa Njombe" alisema Erasto Ngole katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe

Ameongeza kuwa "Zipo tetesi mtaani kwamba Chama cha Mapinduzi kinavurugana na kuna Clip mtandaoni inaonesha kuna baadhi ya maeneo kuna matatizo.Chama cha Mapinduzi ni Chama Kikubwa na kina watu wengi kwa hiyo unavyokuwa na kundi kubwa kama hilo ni lazima utegemee migongano"aliongezaErasto Ngole Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe

Vile vile amesema"Kulikuwa na mgongano kata ya Mji Mwema halmashauri ya mji wa Njombe na mgongano katika siasa ni kitu cha kawaida,niwadhibitishie mgongano unakwenda kuondoka na tunabaki wa moja,sisi tunasuruhisha migogoro ya kimataifa kwa hiyo mgogoro wa Mji Mwema ni mdogo kesho (Leo) unaenda kuisha kwasababu wote waliogombea ni wana CCM"alisema Erasto Ngole katibu wa Siasa na Uenezi Njombe

Aidha Chama Hicho Kimefunga Zoezi la Uchukuaji Fomu Kwa Wagombea Wao Wa Ubunge Katika Jimbo la Lupembe Mkoani Njombe Ambako Mgombea wa Jimbo Hilo Bwana Edwin Enosy Swale Amesema Amedhamiria Kwenda Kutatua Changamoto Mbalimbali za Wakazi wa Jimbo Hilo Ambazo Zimekuwa Mwiba Kwa Miongo Mingi Sasa,huku akishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kumpa ridhaa.

"Natoa shukrani kwa Chama changu cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa CCM kwa kunipa heshima kubwa ya kuwakilisha Chama katika Jimbo la Lupembe kwa hiki ndio Chama cha Watanzania,CCM imedhihirisha ukiwa maskini au mwenye fedha unapata fursa ya uongozi mradi una sifa"alisema Edwin Swale mgombea wa Ubunge Jimbo la Lupembe mkoani Njombe akishukuru baada ya kuchukua fomu ya Uchaguzi

Aidha kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Lupembe amesema Jumla ya vyama vitatu vya CHADEMA,ACT na CCM wamechukuwa fomu za kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo.

Agosti 25 Mwaka Huu ni Siku ya Urejeshaji Fomu za Wagombea wa Vyama Vyote Nchini kwa Ngazi ya Udiwani na Ubunge Kabla ya Kuanza Kwa Kipyenga Cha Kampeni Hapo Agosti 29 Mwaka Huu.


Post a Comment

0 Comments