SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) rasmi imeruhusu kuendelea kwa Shughuli zote za Michezo pamoja na kuruhusu Mashabiki kuingia Viwanjani na kuwataka kuendelea kuchukua tahadhari ya maradhi ya Covid 19.
SMZ ilitoa katazo la kuzua shughuli mbalimbali ikiwemo michezo na kuzuia mashabiki kuingia viwanjani kutokana na mripuko wa homa kali ya mapafu (Covid 19) inayosababishwa na virusi hatari vya corona.
Ikumbukwe kwamba June 5, 2020 SMZ iliregeza masharti na kuanza kuruhusu kwa baadhi ya shughuli kurejea huku Ligi kuu soka Zanzibar pekee iliruhusiwa kutumuia vumbi katika viwanja tofauti tofauti bila ya kuwa na mashabiki.
Akitoa taarifa rasmi ya Serikali kwa vyombo vya Habari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali imefikia uwamuzi huo kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa cha uogonjwa wa Covid 19 uliukumba Zanzibar na ulimwengu kwa ujumla.
"Kuanzia sasa shughuli zote za michezo ambazo zitahusisha ligi kwa madaraja yote yataruhusiwa kuendelea kuchezwa huku mashabiki nao wakiruhusiwa kuingia viwanjani" alisema Waziri Aboud.
Pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imefungua rasmi vyuo vya Qur-ani (Madrasa) na elimu zinazotolewa na taasisi nyengine za kidini zikiwemo madarasa za watu wazima misikitini, madarasa za akina mama, na shughuli zote za mikusanyiko za elimu ya kidini.
0 Comments