Na Amiri Kilagalila,Njombe
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Makete Profesa Norman Sigala King
Pamoja na Gerson Lwenge Wanging'ombe wamekiandikia barua Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mkoa wa Njombe kukata rufaa inayopinga
matokeo ya kura za maoni ya Ubunge kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi
mkuu wa Octoba 28,2020.
Katibu wa siasa,Itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto
Ngole amewaeleza wanahabari jana mara
baada ya kukamilika kwa mchakato wa kura
za maoni upande wa viti maalum (UWT) uliofanyika katika ukumbi wa Green City
mjini Makambako,Ngole amesema wamezipokea rufaa hizo na watazifanyia kazi kwa
kutenda haki kwa kuzingatia taratibu za Chama hicho.
“Hakujawa na malalamiko mengi japo tumepokea rufaa
kutoka jimbo la Makete Mh,Norman Sigala amekata rufaa mbunge ambaye alikuwa
anamaliza muda wake.Lakini pia tumepokea barua kutoka Wanging’ombe kwa
Mh,Gerson Lenge naye inaonyesha hajaridhishwa na kilichotokea na kinachoendelea
sasa ni kufuata taratibu za Chama,vipo vikao vinavyosikiliza rufaa” alisema Erasto Ngole katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa
Njombe
Vile Ngole amesema mara baada ya kukamilika kwa mchakato
wa kura za maoni kwa upande wa wabunge wa viti maalum kupitia Jumuiya ya umoja
wa wanawake (UWT) mkoa wa Njombe uliowapa ushindi Mbunge wa viti Maalum aliyemaliza muda wake Bi,Neema Mgaya pamoja
na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt,Pindi Hazara Chana
kwa kupata kura Neema Mgaya -239,Pindi
Chana -202 na Rebecca Nsemwa-151.Huku
akifafanua kuwa kinachofuata kwa sasa ni kura za maoni kuwapata madiwani wa
kata na viti maalum.
Kwa upande wa kura za maoni jimbo la Makete lililosababisha
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Prof,Sigala kukata rufaa,Matokeo ya washindi wa
mwanzo yaliwapa ushindi Festo Sanga-116,Norman Sigala-89,Ignatio Mtawa -86 huku
wilayani Wanging’ombe Enock Kiswaga-175,Gerson Lwenge-159 na Festo Dugange-92.
Aidha mara baada ya matokeo ya kura za maoni
jimbo la Makete,Sigala alinukuliwa na baadhi ya vyombo akifafanua uchaguzi huo
kugubikwa na vitendo viovu ikiwemo vitendo vya rushwa.
“Nikawasiliana na TAKUKURU wilaya ya Makete
nikampigia simu afisa nikamueleza hali halisi kwamba nimeona mimi na
nikamuandikia meseji kwamba hawa watu wanafanya fujo ni vizuri waangaliwe na
afisa akaniambia anashughulika na usimamizi ulikuwa haujaanza”amenukuliwa
Sigala.
0 Comments