TANGAZA NASI

header ads

Uchaguzi wa Bolivia waahirishwa kwa sababu ya corona


Uchaguzi mkuu wa Bolivia umeahirishwa hadi Oktoba 18, huku janga la virusi vya corona likiwa linaendelea kulitikisa taifa hilo la Amerika Kusini.

Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea mivutano kati ya serikali ya mpito ya siasa za kihafidhina iliyo madarakani na chama cha kisoshalisti cha rais wa zamani Evo Morales.

Mkuu wa tume ya uchaguzi amesema jana kwamba uchaguzi huo uliokuwa ufanyike Septemba 6 umesogezwa mbele ili kulinda usalama wa wapiga kura.

Kufuatia uchaguzi wa mwaka jana uliosababisha maandamano kuenea kote nchini humo, pamoja na kujiuzulu kwa Morales, kura hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa kisiasa wa taifa hilo lenye idadi ya watu wapatao milioni 11.5.

Post a Comment

0 Comments