Na Amiri Kilagalila,Njombe
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally
Kasinge ameishukuru serikali na Chama cha Mapinduzi kupitia Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kumuamini na kumpa nafasi ya uongozi kama mkuu wa
wilaya hiyo kwa miaka minne mpaka hapo jana July 7 nafasi yake ilipochukuliwa
na kiongozi mwingine.
Kasinge ametoa shukrani zake kupitia vyombo vya
habari wakati akiwaaga wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe na viongozi wote wa
Chama na Serikali.
“Namshukuru sana Mh,Rais alipoendelea kuniamini na
kuniteua kuwa mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe tangu tarehe 26 mwezi wa 6 mwaka 2016 kwa hiyo nimeweza
kutumika kwa miaka minn na siku kama 11,kwa hiyo nina kila sababu ya kumshukuru
Mh,Rais kwa kuniamini na kubaki katika nafasi kwa kipindi chote hicho,lakini
pili ninamshukuru kwa kuendelea kuniamini kubaki kwa kipindi hicho chote mpaka
pale ambapo amenipa kibali kwa kile ambacho nimeomba ili nikashughulike na
maswala mengine ya kisiasa”alisema Kasinge
Aidha amekishukuru Chama cha Mapinduzi
“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipokishukuru Chama change
cha Mpainduzi,ndicho ambacho kimenilea katika tasnia ya uongozi na maadili ya
uongozi,uzalendo,utiifu ,uchapa kazi na uwajibikaji.kwa kweli nakishukuru sana
Chama cha mapinduzi ndicho ambacho kimenifikisha hapa,na nitaendelea kuwa
mwaminifu katika Chama changu cha Mapinduzi na kuendelea kuwa mwaminifu katika
nchi ya ngu”
Aishukuru serikali ya mkoa wa Njombe
“Niishukuru sana serikali ya mkoa wa Njombe ambapo nimetumika wakuu wa mikoa
wawili na nimekuwa na Mh,Christopher Ole Sendeka Kaka yangu tumefanya naye kazi
vizuri sana na alinilea katika maadili ya kazi,uzalendo na utiifu katika
nchi,kwa kweli ni kiongozi wa namna yake wa kuigwa”alisema Kasinge
Hata hivyo Kasinge amewashukuru wananchi wa
Wanging’ombe,watumishi serikali na Chama kwa kuwa malengo
waliyokusudia ya kuyafanya kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi
yamekamilika kwa asilimi 90 mpaka 100.
Rais wa
jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli jana Julai 07,2020 alifanya
uteuzi wa Mkuu wa wilaya mmoja na wakurugenzi wa Halmashauri watano katika
mikoa mbalimbali.
Rais Magufuli alimteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Wanging’ombe Mkoani Njombe akichukua nafasi ya Ally Kasinge,ambapo kabla ya
uteuzi huo Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za
Mitaa huko Mkoani Songwe.
0 Comments