Na Amiri Kilagalila,Njombe
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani
Njombe Ndugu Ally Kasinge ametangaza nia
ya kuingia katika mchakato wa kula za maoni wa kumpata mgombea wa ubunge kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama cha
Mapinduzi jimbo la Kilwa Kusini
Kasinge ameweka wazi nia yake mapema siku ya leo
wakati akizungumza na vyombo vya habari kwa minajili ya kumshukuru Mh,Rais
Magufuli kwa kumuamini na kumteua kusimamia halmashauri ya wilaya ya
Wanging;ombe mpaka siku ya jana July 7
alipoteuliwa Lauteri Kanoni kuwa mkuu wa wilaya hiyo.
“Kabla ya hotuba ya Rais baada ya kuapisha wateule
wale ambao aliwaapisha majuzi,ilikuwa ni ngumu kidogo kutafsiri maana halisi ya
Mh Rais anakusudia nini kwa sisi wateule wake”alisema Kasinge
“Mimi binafsi tayari nilikuwa ninamatamanio ya
kufikiria kufanya utaratibu wa kwenda kwenye Chama changu cha Mapinduzi kwenda
katika mchakato kwa kura za maoni,lakini Mh Rais aliweka wazi kwamba yeye hazuii wateule wake kwenda kuomba kibali
au kuomba ruhusa na kuingia katika mchakato wa kisiasa.na alichokuwa
anakielekeza kwamba watu wazingatie taratibu waombe ruhusa kwakwe,anatoa ruhusa
na baada ya hapo nafasi ambayo alikuwa amekupa anamkabidhi mtu mwingine”alisema
Kasinge
Aidha amesema kutokana na maelezo ya Mh Rais ya mala
kwa mala juu ya wateule wake haikuwa ngumu kwake kuandika barua ya kuomba
kibali kwake.
“Hatua yangu
ya kuandika barua kwa Mh,Rais kuomba kibali ilikuwa ni hatau ambayo nimeifanya
kwa moyo mkubwa na hasa nikiamini kuwa kazi ambayo amenikabidhi kuwatumikia
wananchi wa Wanging’ombe kwa kipindi
ambacho nimefanya cha miaka minne kwa kifupi nimeifanya kwa ukamilifu wake kama
kulikuwa na mapungufu ni ya kibinadamu lakini hakuna binadamu ambaye ni
mkamilifu”Alisema Kasinge
Vilele Kasinge amemshukuru Mh,Rais kumuamini na
kumuacha katika wilaya hiyo moja ya Wanging’ombe kwa kipindi cha miaka minne.
Katika hatua nyingine Kassinge amesema yuko tayari
kuwatumikia wananchi wa Kilwa Kusini kwa njia nyingine kwa kuwa anaamini
upinzani ulipata nafasi kuanzia mwaka 2010 kutokana na changamoto zilizokuwemo
ndani ya Chama cha Mapinduzi.
“Seleman Bungala maarufu kama Bwege aliingia bungeni
mwaka 2010 na ndio mwaka ambao mimi kwa mala ya kwanza niliingia katika
mchakato wa kura za maoni za Chama cha Mapinduzi jimbo la Kilwa kusini lakini
kutokana na utaratibu ambao haukuwa mzuri kwa wakati huo,ulitoa fursa kwa
wapinzani hasa kwa wakati huo chama cha Cuf kuchukuwa jimbo la Kilwa kusini”alisema
tena Kasinge
Rais wa
jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli jana Julai 07,2020 alifanya
uteuzi wa Mkuu wa wilaya mmoja na wakurugenzi wa Halmashauri watano katika
mikoa mbalimbali.
Rais Magufuli alimteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Wanging’ombe Mkoani Njombe akichukua nafasi ya Ally Kasinge,ambapo kabla ya
uteuzi huo Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za
Mitaa huko Mkoani Songwe.
0 Comments