Wananchi wa Kijiji (Mtaa) wa Mbawala Chini Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara kwa sasa wataondokana na changamoto ya kupata matabiabu mbali na eneo lao mara bada ya kukamilika kwa Zahanati iliyojengwa katika kijiji (Mtaa) huo.
Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani Emanuel Mwaigobeko amsesma kuwa zahanati hiyo kwa sasa imekamilika kwa 98% na kilichobaki ni usajili ili ianze kufanya kazi.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa sasa amishaandika barua kwenda kwa katibu Mkuu Wizara ya Afya ili waweze kuapata usajili huku tayari wamishatengwa watumishi watatu,daktari mmoja na wauguzi wawili kwa ajili ya kuanza kutoa huduma katika Zahanati hiyo.
Kabla ya kukamilika kwa zahanati hiyo wananchi wa Mbawala Chini walikuwa wanapata huduma hiyo kwenye kituo cha Afya Naliendele ambapo kuna umbali wa Zaidi Km 5.
Ujenzi wa Zahanati hiyo umetokana na Mapato ya ndani ya Halmshauri hiyo huku wananchi wakitoa nguvu kazi zao na hatiamae imekamilika na sasa ipo tayari kutoa huduma ya Afya.
0 Comments