Rais mpya wa Malawi Lazarus Chakwera amefutilia mbali sherehe zilizopangwa za uhuru na vilevile amepunguza pakubwa sherehe za kuapishwa kwake, kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Malawi imerekodi visa 1,613 vya maambukizi ya corona na haijaweza vizuizi. Katika hotuba yake siku ya Jumapili, Rais Chakwera alisema sherehe ya kuapishwa kwake sasa itafanyika katika kambi ya kijeshi na watu 100 pekee walioalikwa ndio watahudhuria.
Chakwera alishinda uchaguzi wa rais uliorudiwa Juni 23 kwa kupata asilimia 58.5 ya kura, dhidi ya aliyekuwa rais Peter Mutharika.
Hatua ya kupunguza sherehe hizo imepunguza furaha ya watu waliotaka kusherehekea ushindi huo wa kihistoria, baada ya mahakama kufutilia matokeo ya uchaguzi wa mwaka uliopita ambapo Peter Mutharika alitangazwa mshindi.
0 Comments