Na Erasto Mgeni,Njombe
Tume ya taifa ya uchaguzi NEC
imehitimisha mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo watumishi 126 kutoka
mikoa mitatu ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania watakaohusika katika mchakato
mzima wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kufunga
mafunzo hayo yalitolewa kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa
uchaguzi,maafisa uchaguzi na Ugavi kutoka mikoa ya Njombe,Ruvuma na Iringa
kamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji Marry Longway amesema uwezo waliojengewa
ukatumike ipasavyo katika kutekeleza majuku yao bila kuvunja sheria ,taratibu
na kanuni za uchaguzi.
“Nina amini mafanikio katika
mafunzo haya yanabashiri uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoweza
kujitokeza katika mafunzo kwa watendaji ngazi ya kata na vitu vya kupiga kura
kadri hatua yautekezaji wa uchaguzi kwa namna nzuri na uelewa mpana”alisema
Jaji Marry Longway
Katika hatua nyingine Jaji Longwaiy ameagiza watumishi hao kwenda kuipeleka elimu hiyo kwa wasimamizi wa uchaguzi
wa uchaguzi ngazi ya kata na vituo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa
weledi katika kipindi chote cha uchaguzi.
“Jukumu lililo mbele yenu ni kutoa
mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata na baadaye mtatoa mafunzo kwa
makarani waongozaji,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi kutoka katika halmashaui
zenu”aliongeza Merry Longway
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
akiwemo Iddy Mponda,Lucy Komba na Hamad Njovu wanasema mafunzo hayo yametolewa
katika muda muafaka na kuahidi kwenda kusimamia zoezi la uchaguzi kwa umakini
na kuzingatia misingi na taratibu ili kupata viongozi bora wa kuwatumikia
watanzania katika kipindi kingine cha miaka 5.
“Mafunzo tuliyoyapata kwanza
yametujengea uelewa wa kutosha hususani kwenye sharia yenyewe ya uchaguzi
lakini pia taratibu zinazotkiwa kufuatwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru
na haki”alisema Iddy Mponda


0 Comments