Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mwanasheria mwandamizi wa mamlaka ya mawasiliano
Tanzania (TCRA) Dkt,Philip Filikunjombe amejitokeza ofisi za Chama hicho wilaya
ya Ludewa Mkoani Njombe na kuchukuwa
fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho
kugombea ubunge wa jimbo la Ludewa.
Filikunjombe
Amekuwa mtia nia namba 8 kuchukuwa fomu mapema asubuhi ya leo July 7
mara baada ya pazia la uchukuaji wa fomu ndani ya chama hicho kufunguliwa huku
watia nia kadhaa kutangulia akiwemo Mbunge Deo Ngalawa aliyemaliza muda wake.
Bakari Mfaume ni katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM
wilaya ya Ludewa,amesema iadadi ya wgombea waliofika kuchukuwa fomu ya Ubunge
wamefikia 8 na wengine wakiendelea kujitokeza licha ya kuwa leo ni siku ya
mwanzo huku fomu za udiwani zikitolewa kwenye kata husika.
“Watu wamejitokeza pamoja na kwamba leo ni siku ya
mwanzo na zoezi la kuchukuwa fomu za udiwani wa kata zinafanyika kwenye kata
zenyewe.lakini kwa udiwani viti maalumu katibu wa UWT wilaya ndiye
anayeshughulikia kuchukuwa hizo fomu na mpaka sasa zoezi limeanza na
linaendelea vizuri”amesema Mfaume
Aidha Katibu emepiga ametoa wito kwa wgombea
kuendelea kufuata sheria na utaratibu wa Chama hicho ikiwemo wanachama
kutoruhusiwa kufika katika ofisi na mbwe mbwe za aina yoyote.
“Yako mambo ambayo haturuhusu na mambo ambayo tuna
ruhusu,katika uchaguzi huu wa nadani wa kumoata mgombea haturuhusu mwanachama
kusindikizwa na watu,kwasababu huu ni uchaguzi wa ndani na sisi tunaamini
wanachama wote ni sawa lakini vile vile tunakataza kufanya kampeni za aina
yoyote kuanzia kuweka katika mitandao au kuwa na vipeperushi au kuwatembelea
wanachama”aliongeza katibu.
Wakati zoezi hilo likiendelea wilayani Ludewa
taarifa zinaeleza kuwa katika majimbo mengine ya uchaguzi mkoani Njombe likiwemo
jimbo la Makete kwa mujibu wa katibu wa chama hicho wilaya wamefika wagombea 20,Jimbo
la Njombe mjini wagombea 8 huku jimbo la Wanging’ombe wakiwa wamefika wagombea 17
na zoezi linaendelea.
Aidha wakati zoezi hilo kwa Chama cha Mapinduzi likionekana
kuendelea vizuri mkoani Njombe,kituo
hiki kimefika katika ofisi za Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wilaya
ya Ludewa na kushuhudia wajumbe wa chama hicho wakiendelea na zoezi la kura za
maoni za kumpata mgombea wao ambapo amepatikana mmoja pekee atakayepigiwa kura
za ndio au hapana.
0 Comments