Na Omary Mngindo, Bagamoyo
Julai 30
WILAYA ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, inakabiliwa na upungufu ya vyumba vya madarasa 139 vya shule ya msingi, sekondari vyumba 34 na mabweni 32 kwa ajili ya wanafunzi kike.
Hatua hiyo inatokana na kufanya vizuri kwa miaka 3 mfululizo, ikishika namba moja darasa la saba, kidato cha 2 na 4, ukiongeza juhudi kubwa za Rais Dkt. John Magufuli za elimu bure, ambayo imekuwa chachu kubwa kwa wazazi kupeleka watoto wao shule.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Zainab Kawawa, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo alisema upande wa mabweni mkazo unewekwa kwa wasichana, li kuwapunguzia changamoto za mitaani, ndipo akaanzisha benki ya matofari.
"Tumeshaanzisha benki hiyo ipo Gereza la Kigongoni, tumepeleka mashine ya mkono, vibao na mifuko ya saruji, pale tuna vijana wanaotumikia adhabu mbalimbali, nasi tumeunga mkono kauli ya Rais ya kuwatumia walioko Magereza kujihisisha na shughuli za uzalishaji," alisema Kawawa.
Aliongeza kuwa mbali ya sekta ya elimu, pia malengo ya kuwepo kwa benki hiyo ni kuhalikisha wanaunga mkono miradi ya majengo ya serikali, yanayoibuliwa na wananchi hatimae wao kuiongezea nguvu kwa kupeleka tofari hatimae miradi husika kukamilika.
Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kigongoni Joseph Siwale alisema kuwa kwa kutumia nguvukazi waliyonayo kikosini hapo, wanendelea na kazi ya ufyatuaji wa tofari, huku akieleeleza kwamba kazi inakwenda vizuri.
Siwale alisema kwamba katika Gereza hilo kuna kisima kikubwa cha maji cha uhakika, kinachochelewesha kuendelea kwa zoezi hilo, huku akielezea upungufu wa mifuko ya saruji, ambapo amewaomba wadau kujitolea magari kwa ajili ya kusomba mchanga, wengine wapeleke mifuko ya saruji.
"Tumepewa jukumu la kutengeneza matofali, changamoto yetu ni kutokuwa na gari la kuleta mchanga hapa saiti, tunalo gari moja tu la Magereza, pia tumeishiwa saruji kama alivyosema Mkuu, tunawaomba wadau watuunge mkono, tulikuwa na mifuko 167 tumefyatua matofari 4,310," alisema Siwale.
0 Comments