Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wasaidizi wa kisheria nchini wameelezwa kuzingatia
maadili katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wahitaji ili waweze
kupata nafuu na haki inayohitajika kwa mujibu wa sheri.
Wito umetolewa na katibu mkuu wa wizara ya katiba na
sheria Prof.Sifuni Mchome wakati akizindua kamati ya uratibu wa shughuli za
msaada wa kisheria mkoa wa Njombe.
“Katika kazi ni wajibu kuhakikisha maadili
yanazingatiwa,maadili katika maeneo mbali mbali,maadili katika ushauri,kupeleka
kesi mahakamani na maadili katika mahusiano yetu na watu ambao tunawahudumia,na
mtoa msaada wa kisheria hawezia akawa mchonganishi”alisema Prof.Sifuni Mchome
Aidha Mchome amesema lengo mojawapo la serikali kuwa
na wasaidizi wa msaada wa kisheria ni
kusaidia katika utetuzi wa migogoro inayojitokeza katika jamii pamoja na
kuhakikisha uwepo wa utawala bora.
Naye mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameiomba wizara ya
katiba na sheria kuongeza nguvu katika kuzisimamia asasi zinazotoa elimu
kutokana na uwepo wa asasai zinazofanya kazi isiyokuwa na afya kwa taifa.
“Kwa muda mrefu huko nyuma asasi hizi zingine
zilikuwa zikifanya kazi ambazo hazina afya kwa ustawi wa nchi na wengine
wamekuwa ni madalali wa kusimamia maslai ya nchi zingine za ughaibuni”alisema
Ole Sendeka
Kaimu aifisa maendeleo ya jamii mkoa wa Njombe
Farahani Kanyenda,amesema wasaidizi na watoa huduma za msaada wa kisheria
wamekuwa na msaada mkubwa kwa jamii na kuwezesha idadi ya watu waliopata
huduma ya msaada wa kisheria kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Mei 20 kufika 8282
kwa upande wa madai,19 kwa upande wa Jinai,26 kwa upande wa matunzo huku watoto
waliopata msaada wa kisheria wakiwa 42.
Erasto Mkiwa ni mratibu wa shirika la PAD na Geofrey
Kaduma ni mkurugenzi wa kituo cha msaada wa sheria Njombe,wanasema licha ya
uwepo wa changamoto katika shughuli zao lakini wanaamini kamati iliyoundwa
itasaidia kuwafikia zaidi wananchi wenye migogoro mbali mbali.
“Kwa kupitia kamati hii itatusaidi kuwafikia zaidi
wananchi kwasababu ni sehemu mojawapo ya kurahisisha mawasiliano na kupitia
wadau tuliopo ni rahisi kuelewa wapi kuna tatizo”Alisema Erasto Mkiwa
0 Comments