Muigizaji wa filamu nchini Steven Mengele, maarufu kama Steve Nyerere, amesema kuwa anawashukuru wale wote wanaomtishia kumuua, hii ni baada ya yeye kuonesha nia ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini kupitia CCM, ambalo liko chini ya Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA.
Steve Nyerere ametoa kauli hiyo leo Juni 19, 2020, jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza nia yake ya kugombea Ubunge na kueleza yeye ndiye atakuwa Mbunge mfupi na machachari kuliko wote.
"Mimi ndiyo Mbunge wa Iringa labda itokee niseme sitaki, nakwenda kurudisha jimbo letu, nawashukuru wanaonitukana na kunitishia kuniua maana wanazidi kunipa nguvu" amesema Steve Nyerere.
0 Comments