Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ikiwa zimebaki siku 9 ili kuvunjwa Bunge la jamhuri
ya muungano wa Tanzania,tayari kuelekea katika shughuli za uchaguzi wa awamu ya
6 hapo Octoba 2020.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka
amewataka wabunge wa vyama vya upinzani kutumia siku chache zilizobaki kupiga
picha na zuria la Bunge pamoja na bendera ya Bunge kwa ajili ya kumbu kumbu kwa
kuwa itakuwa ni vigumu kwao kuingia Bungeni kwa sasa.
Ole Sendeka aliyasema hayo jana wakati akizungumza
na madiwani wa halmashauri ya mji wa Makambako katika kikao chao cha baraza
maalum la kujadili hoja za mkaguzi,mda mchache kabla ya kikao cha kuvunja
baraza hilo.
“Bunge linavunjwa tarehe 19,waambieni wabunge wa
upinzani walioko kwenye mjengo wa Bunge watumie siku hizi kumi kupiga picha
kwenye zuria jekundu la Bunge,watumie siku hizi kumi kupiga picha na bendera ya
Bunge kwasababu Mh,Lowasa alikwishatabili kwamba upinzani ukishindwa 2015
usubili miaka 50”alisema Christopher Ole Sendeka
“Nyanda za juu kusini hakuna jimbo litakalo kwenda
upinzani,na kwa chama kile ambacho kimekuwa kinajinasibu ambacho leo kinafanya
maigizo hata leo (jana) yale ya Dodoma mliyoyasikia nataka niwaambieni kwa
upande wa Tanzania Bara wataliskia tu Bunge” alisema tena Christopher Ole
Sendeka
Sendeka amesema anaamini watanzania wamepata
majawabu dhidi ya vilio vilivyotokana na ufisadi,Rushwa,uonevu,ubadhilifu,mapambano
ya watumishi hewa,mishahara hewa,wanafunzi hewa kutokana shughuli kubwa
iliyofanywa na Rais Magufuli ili kurejesha imani kwa watanzani dhidi ya Chama
cha Mapinduzi pamoja na kujenga miundombinu mikubwa ikiwemo Reli ya kisasa.
Katika swala la hoja za mkaguzi katika halmashauri
ya Makambako,Ole Sendeka ametoa pongezi kwa halmashauri hiyo kuendelea kupata
hati safi kwa miaka 7 mfululizo pamoja na kupunguza hoja za mkaguzi kutoka 50
mpaka 28,huku akiitaka halmashauri kuendelea kuwa mabingwa wa kuzuia hoja na
sio kutengeneza hoja za mkaguzi.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Makambako Deo
Sanga ametumia nafasi hiyo kumtaka mkurugenzi kusimamia vizuri kazi zilizokuwa
zikifanywa na madiwani mpaka mwezi wa 11 litakapoundwa baraza jipya.
“Baraza hili ni la mwisho kazi zote zilizofanywa na
madiwani hawa zinaachwa kwa mkurugenzi ambao madiwani kwa muda mfupi watakuwa
ni hawa wakuu wa idara ni imani yetu mpaka tutakapo ludi mwezi wa 11 baada ya
uchaguzi tuone shughuli zimesimamiwa vizuri”alisema Sanga mbele ya Mkurugenzi
wa halmashauli Poul Malala
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana
Mfikwa amesema kama madiwani wamefanya kazi kubwa katika halmashauri hiyo hivyo
kilichobaki sasa ni kwenda kujipanga upya katika swala la uchaguzi.
Baadhi ya madiwani akiwemo Emmanuel Fute ambaye ni
diwani wa kata ya Kitandililo na Jackson Kivambe diwani wa kata ya Kivavi wawamesema
wanakwenda kumaliza muda wao lakini wanaiomba serikali ya mkoa kuzirejeshe
fedha za wananchi zilizokusanywa na serikali kutoka mikononi mwa wachache
waliohujumu vyama vya ushirika na Saccos ikiwemo benk ya wananchi Njocoba ili
zikatumike kwa maendeleo ya wananchi,Huku mkuu wa mkoa wa Njombe akiahidi
kurejesha fedha hizo zaidi ya bilioni 5 kabla ya kumalizika kwa mwezi July.
0 Comments