Na Amiri kilagalila,Njombe
Naibu waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Elias kwandikwa amemuagiza
mkandarasi anayejenga barabara ya Njombe kuelekea wilayani Makete kipande cha Njombe-Moronga
kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa
kipande hicho na kuhakikisha imekamilika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Agizo hilo amelitoa wakati akikagua ujenzi wa
barabara hiyo katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo amesema anataka
kuona ujenzi huo unakamilika ili wananchi waendelee kunufaika na barabara hiyo
kwa kuwa serikali imeshawalipa fedha makandarasi wote nchini.
“Mkandarasi afanye kazi kadri itakavyowezekana
barabara hii kipande hiki ifikapo mwezi Octoba iwe imekamilika nafikiri hakuna
mashaka kwasababu kazi imefanyika.Na sisi kama serikali tumejipanga vizuri
kuendelea kuwalipa wakandarasi ili tuhakikishe watanzania wanafurahi matunda ya
koi zao”alisema Kwandikwa
Meneja wa Tanroad mkoa wa Njombe mhandisi Yusuph Mazana
amesema tayari mkandarasi huyo ameshalipwa fedha zote na kazi zimekuwa zikienda
vizuri licha ya mkoa wa Njombe kuwa na vipindi virefu vya mvua huku mhandisi
mshauri wa barabara hiyo Lusekelo Kijalo
kwa niaba ya mkandarasi wa barabara hiyo amesema ni lazima wakamilishe ujenzi
huo kama mkataba unavyoelekeza.
Christopher Ole Sendeka ni mkuu wa mkoa wa Njombe
ambaye amesema endapo barabara hiyo itakamilika hadi kuungana na mkoa wa Mbeya
itawasaidia sana wakulima kusafirisha mazao yao kwenda katika uwanja wa ndege
wa Songwe.
“Tanzania tunaweza ndio maana Mh.Rais amethibitisha
kwa vitendo kujenga barabara hii itakayokuwa na km 107 kwa kiwango cha lami
kutoka Njombe-Moronga na sehemu ya pili kutoka Moronga kwenda Makete.Lakini nia
ni kuendeleza barabara kutoka Iwawa makao makuu ya wilaya ya Makete kwenda
Isyonje mkoa wa Mbeya ambayo itawezesha wananchi wa mkoa wa Njombe kusafirisha
mazao yao ya kilimo kupitia uwanja wetu wa Ndege wa Songwe”alisema Ole Sendeka
0 Comments