Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ametangaza kuwa mwaka huu hakutokuwa na ibada ya hijja hii ni kutokana na kauli iliyotolewa wiki hii na serikali ya Saudi Arabia kutokana na janga la Corona.
Ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.
Mufti Zubeir amezitaka madrasa zote nchini kuanzia sasa kurejesha shughuli zote za madrasa nchini huku zikizingatia taratibu zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya nchini.cv
0 Comments