TANGAZA NASI

header ads

Makambako:Watoto kutoruhusiwa kuingia sokoni ili kuepuka Corona



Na Elizabeth Kilindi,Njombe.

Afisa ustawi wa jamii halmashuri ya Mji Makambako Masinde Masinde,amesema wamelazimika kuandika barua kwa uongozi wa masoko katika halmashauri hiyo kutoruhusu watoto kuingia sokoni ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Afisa ustawi Masinde aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Njombe Press Club Blog,ambapo alisema bado kuna changamoto kipindi hiki cha likizo watoto kuonekana kwa wingi maeneo ya sokoni huku wengine wakitumikishwa

"Ukiangalia mji wetu wa Makambako maeneo ya sokoni unakuta watoto wamejazana  wengi wanazunguuka tu,na baada ya kuliona hilo katika kikao chetu cha robo tumechukua uamuzi kwamba mkurugenzi atawaandikia barua uongozi wa masoko maana imeonekana sehemu ya soko inawavutia watoto wengi"alisema Masinde.

Aliongeza kuwa"wakienda pale wanapata shughuli ndogo za kuweza kufanya kazi,kupata chochote kwa hiyo tunawandikia barua uongozi wa masoko yote kwamba watoto wasiruhusiwe kuingia sokoni na mtu yoyote atakaempa  kazi mtoto akibainika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ya mtoto"alisema Masinde.

Aidha Masinde pia  alisema bado kunachangamoto ya wazazi kutowangalia watoto wao hali inayopelekea watoto hao kuzurura hovyo.

"Pamoja na kwamba serikali imeamua watoto wabaki nyumbani kwa sababu ya kuzuia kuenea kwa  virusi vya corona lakini bado wazazi wameshindwa kuangalia watoto wao kwa sabbau mwisho wa siku wamekua watoto wa kuzagaa zagaa tu mitaani"alisema.

Masinde pia aliitoa wito kwa jamii kuongeza juhudi katika swala zima la  ulinzi wa watoto ili kuwakinga na majanga mbalimbali ikiwemo la kuambukizwa virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments