KITENDO cha nyota wa Klabu ya Yanga, Bernard
Morrison kuvaa barakoa kwa muda wote aliokuwa kwenye mazoezi ya kikosi,
kimemkuna daktari wa kikosi hicho, Shecky Mngazija ambaye hakusita kusifu
usikivu wa nyota huyo raia wa Ghana.
Tofauti na wachezaji wengine waliofi ka
mazoezini hapo ambao walivua barakoa zao wakati wa mazoezi lakini Morrison
aliendelea kuivaa hadi alipoondoka uwanjani hapo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mngazija
alisema Morrison alionyesha mfano mzuri wa kuzingatia maagizo ambayo wachezaji walipewa
ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona wanapokuwa mazoezini.
“Tuliwapa wachezaji wote utaratibu mzima
wanaopaswa kuuzingatia ili kuendelea kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi
vya Corona wanapokuwa kwenye mazoezi, kwa upande wangu kwenye mazoezi haya,
Morrison ndiye aliyejitahidi kufuata utaratibu huo kwa asilimia nyingi zaidi
kwa kuvaa barakoa yake muda wote wa mazoezi.
“Lakini pia nawapongeza wachezaji wengine
ambao pia walionekana kufuata utaratibu kwa kunawa maji tiririka na sabuni na
kuvaa barakoa zao wakati wanawasili, unajua huu ni utaratibu mpya kidogo kwao,
hivyo wanahitaji muda kuuzoea nasi tunaendelea kuwasisitiza wachezaji wetu.
“Yanga iliyo katika nafasi ya tatu kwenye
msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kujikusanyia pointi 51 katika michezo yake
27, jana iliendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria uliopo Ubungo
jijini Dar.
0 Comments