Na Gabriel Kilamlya,Njombe
Aliyewahi kuwa katibu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Njombe aliyepokelewa nafasi hiyo kwenye chaguzi za ndani za chama hicho mwaka 2019 Ndugu Alatanga Nyagawa,Leo ametangaza kukihama chama hicho na kurejea CCM kwa madai ya kukosekana kwa ajenda ndani ya upinzani.
Vile vile Alatanga amesema hakuna ubishi kwamba Serikali ya awamu ya Tano imepiga hatua kubwa katika shughuli za maendeleo na upinzani umekosa ajenda.
Alatanga ambaye aliwahi kugombea Ubunge katika jimbo la Lupembe mwaka 2010 na kutia nia katika jimbo la Njombe mjini mwaka 2015 kupitia Chadema amepokelewa na viongozi wa CCM kata ya Ikuna ambako ni nyumbani kwake.
Daitan Mhema ni katibu kata na Barnaba Kigahe ni mwenyekiti wa CCM kata ya Ikuna wamekiri kuwa Alatanga amewasumbua sana akiwa upinzani na sasa wanategemea kujenga chama chao kwa pamoja.
0 Comments