TANGAZA NASI

header ads

Wasichana wa shule za msingi hukumbwa na Changamoto kubwa wanapokuwa Hedhi






Na Jackline Kuwanda, DODOMA.

Recho Steven kutoka Shirika la Plan international amesema kuwa wamekuwa wakishughulika na mradi wa usafi wa mazingira Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa jamii zinabadili tabia katika masuala ya usafi wa mazingira kwa ujumla wake kuanzia ujenzi wa vyoo bora ,matumzi ya vyoo bora,unawaji wa mikono ,masuala ya hedhi salama kwa watoto wa kike pamoja na wanawake kwa ujumla.

Akizungumza Siku ya Hedhi  Duniani iliyoadhimishwa May 28,Recho amezungumzia hali ya mila,Tamaduni ambazo zimechangia suala la hedhi kutozungumziwa kwa wazi na kusababisha watoto wa kike kukosa masomo kipindi ambacho wako katika hedhi.

Amesema kuwa watoto wa kike wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwa na miundombinu rafiki ambayo wangeweza kujisitiri vyema pindi wakiwa mashuleni .

Wakati huo huo amesema kuwa mara nyingi watoto wanakosa masomo wakati wa hedhi ni wale ambao wako katika shule za msingi .

kutokana na hali hiyo pia amesema kuwa baadhi ya wazazi wanachangia kwa kiasi kikubwa kwani wengine hufikia hatua ya kumuombea mtoto ruhusa kwa kisingizio kuwa anaumwa.

Post a Comment

0 Comments