Na Amiri kilagalila,Njombe
Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakulima
inayopelekea kukuwa kwa sekta ya kilimo na kusaidia kuongezeka kwa pato la
mkulima na Taifa,Kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Uyole,wanasema lengo la
kituo kwa sasa ni kuona mkulima Mahiri na anayefanikiwa katika maisha kutokana
na kilimo bora na chenye tija.
Amebainisha hilo Dkt.Tulole Lugendo Bucheyeki
mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole,wakati akikagua maendeleo ya shamba la mkulima
wa Mahindi kupitia mradi wa kuboresha kilimo na maisha ya mkulima kwa kutumia mbegu
bora lililopo kijiji cha Ilunda kata ya Mtwango wilayani Njombe.
“Lengo la sasa tunataka mkulima aondoke pale alipo
kimaisha,awe mahiri na mkulima huyo tutampima kwa sifa zifuatazo,ambaye atalima
kilimo chenye faida,atajitosheleza kwa chakula,ni mkulima ambaye atazalisha
mazao kwa ajili ya malighafi ya viwandani,awe ambaye anakuwa na chakula chenye
lishe na ambaye hata teteleka na mabadiliko ya hali ya hewa” Dkt.Tulole Lugendo
Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole
Amesema kwa sasa kituo cha Uyole kina aina zaidi ya
8 ya Mahindi zitakazomuwezesha mkulima wa sehemu mbali mbali nchini kufaidika
yatakapotunzwa,huku akibainisha kuwa awali walikuwa na mbegu na mbegu kwa ajili
Nyanda za juu kusini tofauti na sasa.
“Tuna aina zaidi ya nane ya mbegu za Mahindi ambazo
zinaweza zikapandwa sehemu mbali mbali,mwanzoni yalikuwa yanapandwa Nyanda za
juu kusini kwa hiyo sasa hivi yanaweza yakpandwa sehemu mbali mbali” Alisema
tena Dkt.Tulole Lugendo Bucheyeki mkurugenzi wa kituo cha TARI Uyole
Vile vile amesema kituo kina aina zaidi ya 22 za
Maharage huku Soya wakiwa na aina nne.
Lornad Sabula ni mtafiti kutoka taasisi ya utafiti
wa kilimo Tanzania kituo cha Uyole na meneja wa mradi wa Pata Tija,anasema kwa
sasa wanahitaji kubadilisha mtazamo wa kilimo kwa wakulima zaidi ya laki moja
katika mazao ya Mahindi,Maharage na Soya.
“Tunataka mkulima wa Soya ajivunie kuwa mkulima
lakini pia mkulima wa Maharage ajivunie kuwa mkulima wa Maharage sambamba na
mkulima wa mahindi,kwa maana ya sera ya nchi sasa hivi tunaelekea kwenye uchumi
wa viwanda,na viwanda vyetu vitatokana na malighafi yanayotokana na kilimo”alisema
Lornad Sabula
Jafari Mbogela na Anna Wikichi ni wakulima wa kijiji
cha Ilunda wanasema wamepata mafanikio makubwa katika kilimo kutokana na
matumizi ya Mbegu bora za kilimo kutoka kituo cha utafiti TARI,hali ambayo
imewawezesha kupata zaidi ya gunia 50 za mahindi kwa ekari moja tofauti na
awali.
“Kuna mabadiliko makubwa kwenye kilimo kwasababu
zamani tulikuwa tunatumia mbegu moja tu ile ya kienyeji sasa walipokuja
kutufunza wenzetu hawa wa Uyole ukweli mafanikio yapo maana yake na wenyewe
wanakuwa humo humo wanatusaidia cha kufanya”alisema Jafari Mbogela
Mpaka sasa mradi wa kuboresha kilimo na maisha ya
wakulima umefanikiwa kuwafika wakulima elfu hamsini wa moja kwa moja katika
mikoa ya nyanda za juu kusini,huku wengine wakifikiwa kupitia kwa
wagani,maonyesho ya kilimo pamoja vyombo vya habari.
0 Comments