TANGAZA NASI

header ads

WADAU WAPAMBANA KUVUNJA TAMADUNI YA USIRI KWA WASICHANA WANAPOKUWA HEDHI



Na Amiri kilagalila,Njombe

Jamii nchini imetakiwa kuvunja tamaduni ya usiri na kuona  hedhi ni kitu cha kawaida kwa watoto wa kike hali itakayowafanya wasichana kujiamini na kujivunia wanapokuwa hedhi.

Hayo yamebainishwa na kiongozi mkuu wa mradi kutoka shirika la hamble unemployment solution in tanzania Faraja Eliezer ambaye ni mkuu wa idara ya afya na mazingira kutoka shirika hilo,walipofika kituo cha kulea watoto yatima cha Familia ya Upendo Uwemba kilichopo  kijiji cha uwemba kwa ajili ya kutoa elimu juu ya hedhi salama.

Amesema lengo la kufika katika kituo hiki ni kutoa elimu ya hedhi salama kwa watoto wa kike ambao ni yatima,kwani jamii imekuwa ikijitenga kutoa elimu hii kutokana na sababu za kiutamaduni

“Tupo kwa ajili ya kuisaidia jamii kuvunja usiri ambao umekuwa ni utamaduni katika jamii za kiafrika hivyo tunajitahidi kuelimisha watoto wa kike na wakiume pamoja na wazazi ili kuondoa usiri na kuona hiki ni kitu cha kawaida kwasababu bila hedhi mimi na wewe tusingekuwepo” Amesema Faraja Eliezer

Ikiwa leo pia ni siku ya hedhi Duniani,Kabula Kidai msaidizi katika programu maalumu ya Days For Girls Njombe inayohusika na utengenezaji wa Taulo za kike,anasema wamejipanga vizuri kuelimisha watoto wa kike juu ya hedhi salama na kuwataka watoto wa kike kujiamini pindi waonapoona dalili ya hedhi na wasisite kuwaambia walezi wao juu ya hali hiyo.

“Lakini kwa leo tumeanzia hapa na tumeweza kutoa elimu ni jinsi gani kwanza mototo wa kike aone ni kitu cha kawaida,asiwe muoga na ajiamini kwa hiyo tumejipanga kuelimisha watoto,ili watambue dalili kwa watoto wa kiume na wa kiume watambue kwanza dalili za kuanzia kubalehe” Amesema Kabula Kidai

Mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha familia ya upendo uwemba Jenifa Msigwa pamoja na watoto wanaoishi kituoni hapa akiwemo Agness Mtewele wanashukuru kwa msaada na elimu waliyopata juu ya Hedhi salama

“Tunashukuru kwa kuja kutukabidhi taulo za kike na msaada wa Barakoa pamoja na elimu hii waliyotupatia leo”amesema Agness Mtewele

Siku ya Hedhi Duniani huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 28-5 ambapo taasisi ya Days For Girls Njombe licha za kutoa Taulo za kike kwa wasichana wamekabidhi barakoa kwaajili ya kujikinga na virusi vya Corona.

Post a Comment

0 Comments