TANGAZA NASI

header ads

Ufaransa kutangaza mipango ya kulegeza marufuku ya COVID-19


Serikali ya Ufaransa leo inatarajiwa kutangaza hatua mpya za kulegeza vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona kwa kuruhusu kufunguliwa tena kwa mikahawa kwenye maeneo ambako mripuko wa virusi hivyo umedhibitiwa.

Duru mjini Paris zimearifu kuwa waziri mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe ataweka wazi awamu ya pili ya mpango wake wa kufungua tena shughuli za kawaida baada ya mkutano na wajumbe wa ngazi ya juu wa Baraza la Mawaziri.

Chini ya mpango huo, mikahawa kwenye maeneo yenye visa vichache vya COVID-19 itaruhusiwa kuanza kazi mnamo Juni 2, lakini ile iliyopo kwenye maeneo hatari ikiwemo mji mkuu Paris, haitofunguliwa hadi mwezi Julai.

Idadi ya kila siku ya vifo vya wagonjwa wa COVID-19 imeendelea kupungua kote nchini Ufaransa huku takwimu za jana Jumatano zinaonesha watu 66 pekee walikufa kutokana na janga hilo.

Post a Comment

0 Comments