Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Mh. David Mathayo ametoa vifaa vya kunawia mikono katika maeneo yenye watu wengi ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona kwa wananchi Wilayani Same.
Akipokea vifaa hivyo mkuu wa wilaya ya Same amewataka wananchi kufuata maelekezo ya serikali juu ya kujikinga na kuvitumia vifaa hivyo kwa usahihi.
Aidha amempongeza Mbunge huyo kwa kujali afya za wananchi wake na wadau wengine waliochangia; pia amewaomba wadau wengine kuchangia kwani bado kuna mahitaji.
"Mimi nina kata 34 katika Wilaya. Hivyo nitagawa vifaa hivi katika kata zote 34 bila kujali jimbo kwani wote wanahitaji kujikinga" Alisema DC huyo.
Naye Mwenyekiti Wa CCM Wilaya Ndugu Isaya Mngulu aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari, kujikinga na COVID 19.
0 Comments