TANGAZA NASI

header ads

Jeshi la Somalia laua magaidi wengine 7 wa al-Shabaab



Jeshi la Taifa la Somalia limefanikiwa kuangamiza wanachama saba wa kundi la kigaidi la al-Shabaab katika eneo la Hiran, katikati mwa nchi.
Mohamud Hassan Ibrahim, kamanda mkuu wa kikosi cha 22 cha jeshi la Somalia amesema magaidi hao wa al-Shabaab waliuawa jana Jumanne katika operesheni iliyolenga maficho ya genge hilo la ukufurishaji katika eneo la Hiran.

Kadhalika wanachama wengine kadhaa wa kundi hilo wamejeruhiwa katika operesheni hiyo ya jana Jumanne.

Operesheni hiyo imejiri siku moja baada ya jeshi la eneo lenye mamlaka ya ndani la Jubaland kutangaza habari ya kuangamiza wanachama wanne wa kundi hilo la kigaidi katika mji wa Dhobley, Kusini mwa Somalia.

Post a Comment

0 Comments