TANGAZA NASI

header ads

Makonda atoa msaada wa mabati kwa wajane waliokumbwa na mafuriko




VIDEO: RC Makonda atoa msaada wa Mabati na kutoa maagizo kwa Wakuu ...

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo April 30, 2020 ametoa msaada wa mabati yenye thamani ya Tsh. 476m kwa ajili ya Kuezeka nyumba 1,000 za Wajane wa mkoa huo ambazo zimeathiriwa na mafuriko. RC Makonda amewataka pia wananchi waliojenga mabondeni kuhama.

RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.

Aidha RC Makonda amewapa siku 10 Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.

Aidha RC Makonda amesema athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.

Post a Comment

0 Comments