Na,Bilgither Nyoni-Makambako
Baadhi ya wazazi na walezi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe,wametajwa kuwa kikwanzo katika kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona kutokana na kushindwa kuwawekea mazingira rafiki watoto wao ya kujinga na ugonjwa huo badala yake wamekuwa wakizunguka ovyo mitaani.
Baadhi wa wananchi mjini Makambako wamesema bado kunachangamoto ya uwepo wa watoto katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu hususani sokoni,hali ambayo inapelekea wawe hatarini kupata virusi hivyo kutokana na wazazi wao kushindwa kuwasimamia na kuwaelekeza tahadhali ambayo wanatakiwa kuichukua ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa hali ya uwepo wa watoto katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi inasababishwa na wazazi ambao wanaamini kuwa ugonjwa huo unawapata zaidi watu wa mataifa mengine na siyo waafrika.
"Asilimia kubwa ya wazazi tupo bize sana kuhusiana na masuala ya kazi,tumesahau kuwalinda watoto wetu hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa Corona ,tunahangaikia maisha ya watoto wenyewe lakini kama endapo hatutawalinda watoto wetu hawa mwisho wa siku tutawasababishia matatizo makubwa ambayo utatuzi wake utakubwa na wenye gharama kubwa zaidi hivyo wazazi tuanaswa kuona namna gani tunawalinda watoto wetu hawa"alisema Anna Luoga mkazi wa Makambako
Kufuatia hali hiyo,afisa ustawi wa jamii katika halmashauri ya mji wa Makambako MASINDE MASINDE amesema licha ya wazazi kutumia muda mwingi katika shuguli za kiuchumi,lakini wanatakiwa kuona namna ya kuwalida watoto wao.
"Changamoto kubwa ambayo tunayo hapa ya jamii ya mji wetu wa makambako wazazi wamejkita sana katika shughuli za uchumi hatukatai wajikite huko lakini wahakikishe kwamba majkumu yao ya malezi wayatimize na kama wanaona wanamajukumu mazito ya kiuchumi tafuta mzima au mtu anaejielewa akae na wale watoto mpe elimu na yeye pia aelewe nimeachiwa watoto hawa inatakiwa niwaangalie hivyo nawasihi tena jukumu la malezi ya watoto ni takwa la kisheria" amesema Masinde
Naye mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa makambako Dkt ALEXANDER MCHOME amesema kuwa watoto wapo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo ikiwa wazazi na walezi watashindwa kuwaelekeza na kuwasaidia namna ya kuchukua tahadhali ambayo inatolewa na watalamu hasa ya kunawa mikono kila wakati na kuepukana na kukaa kwenye maeneo ambayo yanamkusanyiko wa watu wengi.
0 Comments