Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia Ibrahim Peter mwenye miaka 26 na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo kikuu cha Dodoma akisomea shahada ya Sayansi ya biolojia kwa makosa ya kuandika na kusambaza ujumbe wa kupotosha jamii kuhusiana na Dawa ya Ugonjwa wa Corona katika makundi ya WhatsApp kwakutumia simu yake ya mkononi.
Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika kijiji cha Mnyele wilaya ya Nyasa na miongoni mwa jumbe alizosambaza ni kwamba dawa ya Corona inatakiwa utwange pilipili kichaa sufuria moja halafu changanya na maji ya vikobe vitano na kunywa kutwa mara Saba kwa muda wa siku tatu na siku ya nne chupa ya upupu kisha jipake mwili mzima.
“Kitendo hicho ni upotoshaji na jeshi la polisi hatuwezi kuendelea kuvumilia na taratibu zinakamilishwa na tuweze kumpeleka Mahakamani” ACP Simon Maigwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma
0 Comments