Na Frankius Cleophace Mara.
Jamii Mkoani Mara imeaswa kuendelea kutunza Vyanzo vya Maji ikiwemo Mto Mara ili kuendeleza ikolojia za Mto huo ikiwa ni pamopoja na Kupanda Miti nakuepuka shuguli za kibinadamu karibu na vyanzo hivyo ambazo zimekuwa zikiharibu Mto huo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Canal: Michel Mntenjele katika ufunguzi wa Maadhimisho ya kumi ya siku ya Mto Mara yanayofanyika viwanja vya chuo cha ualimu Wilayani Tarime Mkoani Mara,
Mkuu wa wilaya alisema kuwa katika maadhimisho hayo ambayo yanahitimishwa hii leo Serikali imepanda vigingi 70 pamoja na Miti takribani elfu kumi na tatu kando ya Mto Mara ndani ya mita sitini katika vijiji vya Murito na Kerende ili kudhibiti shughuli za kibinadamui zinazoathiri bonde hilo.
“Nasisitiza viongozi wa serikali katika maeneo ya Murito na kerende pamoja na wananchi kuendelea kulinda na kutunza miti yote ambayo imepandwa ndani ya mita sitini kandokando ya mto Mara ili kuendelea kulinda ikolojia yam to huo” alisema Mkuu wa wilaya Tarime.
Pia Mkuu wa wilaya alisisitiza jamii kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio vya wanyama mbalimbali ili kuona maajabu saba yanayofanya hifadhi hiyo kutambulika Duniani kote ikiwemo tukio la wanyama aina ya Nyumbu ambao uenda kuzalia Nchini Kenya kupitia eneo la Masaimara.
“Watu wengi huwa tunadhani wale wanyama aina ya Nyumbu wakivuka Serengeti wanafika Kenya moja kwa moja siyo kwenye wale wanyama wakitoka hifaddhi ya Serengeti wanaingia kwenye hifadhi hiyo hiyo lakini upande wa wilaya ya Tarime ambapo kuna takribani kilometa kumi na mbili kuingia Masaimara upande wa Kenya hivyo lazima sasa watanzania wajue kuwa Wanyama hawa wanatokea Tanzania kwa asilimia kubwa nakwenda upnde wa Kenya kuzaliana na kasha urejea Tanzani sasa ni moja ya maajabu kati ya maajabu saba kidunia sasa tembelea hifdhi kwa ajili ya kujionea maajabu hayo” alisema Michael Mkuu wa wilaya Tarime.
Kwa upande wake Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwaniaba ya katibu tawala alisema kuwa jamii ione umhimu wa maaadhimisho hayo nakuendelea kuyaenzi yake yote yaliyofanyika kipindi cha maadhimisho hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Katika Maonyesho hayo pia zimeshiriki taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha Sophia Lyimo ni Meneja wa benki ya NBC Tawila la Muaoma Mkoani Mara alisema kuwa wao kama taasisi za kifedha wako bega kwa bega na serikali katika utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima Mikopo yenye bei nafuu ili kujikwamua kiuchumi.
“NBC kama benki tumeshiriki kikamili katika maadhimisho hayo pia tuna akaunti zijulikanazo kuwa Nasi akaunti ambazo hazina makato pia akaunti za wakulima lengo ni kuhakikisha mkulima anakuwa na akaunti ili kutunza fedha ili ziwe salama zaidi” alisema Lyimo Meneja wa NBC Musoma.
Aidha Mwenyekiti wa Halamashauri ya Mji wa Tarime Daniel Komote amewakikishia usalama wa kutosha washiriki wa Maonyesho hayo ambapo anasisitiza suala la jamii kutumia fursa hiyo ya maonyesho ili kujiongezea kipato.
Naye Afisa Uhusiano Bodi ya Maji Bonde la Mto Ziwa Victoria Perepetua Masaga aliongeza kuwa jamii iendelee kushirikiana vyema na serikali za vijiji kulinda sera za Mazingira huku ikiepuka kufanya shuguli za kibinadamu ndani ya mita sitini
Maadhimisho ya kumi ya siku ya Mto Mara yanatarajia kuhitimishwa hii leo ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Maji Juma Aweso na kauli mbili inasema kuwa Tuhifadhi Mto Mara kwa Utalii na uchumi Endelevu.
0 Comments