TANGAZA NASI

header ads

DC Njombe apingana na TRA kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango




Na Amiri Kilagalila,Njombe


Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kubadilisha mfumo wa utoaji elimu kwa mlipa kodi,kuto fuata mlango kwa mlango kwa kuwa utaratibu huo unaweza kukaribisha mazungumzo yenye chembe ya uonevu au rushwa baina ya mfanyabiashara na mamlaka.


Msafiri ametoa agizo hilo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mtwango wilayani humo.


“Ukimfuata mtu mmoja mmoja kwa mtazamo wangu ni kuwaganya na kuwatawala,hii sio namna ya uendeshaji iliyo bora,uendeshaji ulio bora unakuwa wazi.Waite wafanyabiashara wako wote na wanaotaka kuja sema nao lakini unapotembele mtu mmoja mmoja mimi naona sio sahihi na TRA waache hilo”alisema Msafiri.


Aidha ameiagiza halmashauri hiyo kuondoa tozo kero kwa kuwa zinapunguza ongezeko la wafanyabiashara.


“Kama tumekuwa na makusanyo mazuri kwenye halmashauri yetu basi hakuna sababu ya kuwa na tozo kero kwa kuwa zinafanya tunabaki na watu wachache lakini wale wengi wanaofanya tuwe na hilo pato wanakimbia,muende mkaangalie tozo kero ambazo zinadidimiza halmashauri tuziondoe kwasababu sit u kudidimiza halmashauri ila zinatengeneza na ile roho ya chuki”alisema Ruth Msafiri


Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amesema tayari yamekwisha tolewa mapendekezo mbali mbali na kufikishwa kwenye wizara husika ili kuondao tozo kero.


“Yametolewa mapendekezo mbali mbali na maombi kwenye wizara inayo husika ili baadhi ya tozo tuweze kuzipitia ili tupunguze na tuwe na tozo rafiki ambazo hazitasababisha wananchi kukwepa tozo”alisema Hongoli


Wiki kadhaa zilizopita katika kikao cha baraza la ushauri mkoa wa Njombe,George Mapunda ambaye ni meneja msaidizi wa mamlaka ya mapato mkoa upande wa ukaguzi alisema,malaka hiyo ilianza kupita mlango kwa mlango ili kutoa elimu kwa mlipa kodi.


“Tulianza mwezi uliopita kuna timu kutoka makao makuu tukishirikiana waliweza kupita mlango kwa mlango kwa ajili ya kuelimisha na walienda mpaka wilayani Ludewa. Na hata sisi ratiba ya kuwatembelea wadau wetu iko pale pale”alisema George Mapunda

Post a Comment

0 Comments