TANGAZA NASI

header ads

SIMBA DHIDI YA AS VITA, MASHABIKI 10,000 RUKSA UWANJA WA MKAPA

 


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiruhusu klabu ya Simba kuingiza mashabiki kwenye mchezo wao dhidi ya AS Vita kutoka Jamhuri ya Congo.


Mchezo huo wa kundi A, utapigwa Jumamosi tarehe 3 Aprili 2021, kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni.


Akiongea mbele ya waandishi wa Habari hii leo, Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa leo wanafuraha mara baada ya kuruhusiwa kuingiza mshabiki kwenye mchezo huo.


“Leo tumepata habari njema kutoka CAF kuwa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club.


“Hii ni fursa ya kipekee ambayo tumeipata, hakuna timu imeruhusiwa kwa idadi hii, masharti ni mengi na lazima tuzingaitie taratibu walizoweka,” alisema Barbara.


Ruksa hiyo imekuja kufuatia katazo lililowekwa mara ya kwanza ya klabu hiyo kutocheza bila mashabiki kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Merreikh ya Sudan uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.


Kwa upande wa Afisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa hali ya kikosi kipo vizuri na hakuna majeruhi yoyote na wachezaji waliokuwa kwenye timu zao za Taifa wameshaanza kuwasili kambini.

“Kwa mashabiki wetu watu 10,000 ni watu wachache sana. Hatutarajii siku ya mchezo watu wawe bado hawajanunua tiketi sababu siku ya mchezo CAF hawaruhusu tiketi kuuzwa uwanjani.”

“Hakuna namna lazima tupate ushindi kwenye mchezo huu. Hii itakuwa ni DO OR DIE; SEASON TWO na hiyo ndio itakuwa kauli mbiu yetu.” amesema Haji Manara

Post a Comment

0 Comments