MSHAMBULIAJI namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC, Prince Dube amerejea kazini rasmi baada ya kuwa nje kwa muda wa wiki mbili akitibu majeraha ya nyama za paja.
Dube amekuwa na mwendo mzuri ndani ya uwanja akiwapa mabosi na mashabiki wake kile ambacho wanakitarajia kwa kuwa akishindwa kufunga basi atatoa pasi ya bao.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu George Lwandamina ikiwa imefunga mabao 34 baada ya kucheza mechi 24 yeye amehusika katika mabao 13.
Ni mabao 8 ameyatupia Dube na yote akiwa ndani ya 18 huku akitengeneza pasi 5, washakji zake Ayoub Lyanga, Obrey Chirwa na Idd Seleman wamekuwa wakizimalizia pasi zake za mwisho.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa Dube yupo kamili kuendelea kuwatumikia.
Huenda anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utachezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 9 ambapo walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-0 Azam FC na ulikuwa ni mchezo wa Kwanza kwa Azam FC kupoteza msimu wa 2020/21.
0 Comments