Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuriho, ameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Mara , kuhakikisha wanapunguza gharama za miradi, hususani wanapofanya upembuzi yakinifu.
Alitoa agizo hilo akiwa katika ziara wilayani Bunda, akikagua ujenzi wa barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya yenye urefu wa kilometa 121.9, pamoja na kipande cha barabara ya lami kutoka Bulamba-Kisorya (kilometa 51).
Akiwa katika ukaguzi huo, Waziri Chamuriho alisema barabara ya Nansio, ambayo inaanzia Nyamuswa-Bunda hadi Kisorya ni muhimu kwa wananchi wa Wilaya ya bunda, kwamba itafungua fursa nyingi ikiwamo usafirishaji wa mazao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alimpongeza mkandarasi anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo na TANROADS kwa kazi nzuri walioifanya katika ujenzi wa barabara hiyo.
0 Comments