TANGAZA NASI

header ads

Wazee waendelea kukumbukwa ili kupunguza ukali wa maisha



Na Amiri Kilagalila,Njombe

 

Diwani wa kata ya Ludende wilayani Ludewa-Njombe Vasco Mgimba,katika mikutano yake ya  kusikiliza kero kwa wananchi akiwa kijiji cha Maholong'wa ameendelea kukabidhi msaada wa Chumvi na Sabuni kwa wazee ili kupunguza ukali wa maisha.


Mgimba amesema lengo la kutoa misaada hiyo katika vijiji ndani ya kata yake ni juhudi zake za kutoa shukrani kwa wazee wa kata hiyo walioweza kumpa nafasi huku akiomba baraka


Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Ludende kuongeza umoja katika maendeleo ili kupunguza shuruti.


"Tuendeleza umoja na utii bila shuruti kwenye shughuli za maendeleo ili tuepuke polisi na askari mgambo watakao baki na jukumu la usalama wa mali zenu"Diwani wa kata Ludende Vasco Mgimba akiwa kijiji cha Maholong'wa


Vile vile bwana Vasco Mgimba amechangia shilingi 100,000/= kwa wakazi wa kijiji cha Maholong'wa ili kuunga mkono shughuli za ukarabati wa nyumba ya Mganga wa zahanati ya kijiji hicho yenye uchakavu wa miundombinu.


Katika hatua nyingine pamoja na timu yake ya wataalam (Wakuu wa idara) wa kata hiyo ametembelea na kuridhishwa na ujenzi wa vyoo vya kisasa katika shule ya msingi Maholong'wa vilivyofadhiliwa na mdau wa maendeleo mzawa wa kijiji hicho anayeishi Dar es Salaam Ndug,John Mgimba vyenye thamani isiyo pungua Milioni 8

Post a Comment

0 Comments