Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wataalamu wanaoendesha zoezi la kuwabainisha watoto
wenye mahitaji maalum mkoani Njombe wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa
ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi ambazo zitaisaidia serikali
kupanga mipango yake katika kuwasaidia watoto hao.
Wito huo umetolewa na afisa elimu mkoa wa Njombe
GIFT KYANDO wakati wa uzinduzi wa zoezi la kubaini watoto wenye mahitaji maalam
katika mkoa wa njombe ambao umefanyika shule ya msingi kahawa iliyopo kata ya
kitisi makambako,ambapo amewataka wabainishaji hao kufanya kazi kwa ufanisi
mkubwa na pindi watakapokutana na changamoto waziwasilishe kwa wakati ili
serikali iweze kuzitatua.
Afisa elimu huyo mkoa wa Njombe KYANDO amewataka
wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wenye mahitaji maalam ili waweze kufanyiwa
uchunguzi na kubaini mahitaji ya msingi ambayo wanatakiwa wasaidiwe.
“Ninaomba wazazi tushirikiane na serikali watoto
waendelee kukuwa wakiwa na ujuzi,na popote pale ndani ya mkoa wetu mtakapopata
changamoto ya ushirikiano tafadhari ziende kwenye mamlaka husika ili tuone
namna ya kuhakikisha zoezi linakwenda vizuri”alisema Gift Kyando
Awali akisoma taarifa ya uzinduzi wa zoezi hilo
afisa elimu maalum mji wa makambako Exaveria mtega amesema kuwa mkoa wa Njombe
una jumla ya wanafunzi 1064 wenye mahitaji maalumu na shule jumuishi 112m na
kueleza kuwa mpango huo utaenda kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa mkakati wa
kutowasaidia watoto wenye mahitaji maalum.
Hata hivyo wazazi wa watoto wenye ulemavu mjini
makambako wamesema kuwa mpango huo wa kubainisha watoto wenye mahitaji maalum
utasaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa watoto ambao wamekuwa wakifichwa na
kukosa haki zao za kimsingi ikiwemo elimu.
0 Comments