Mkuu wa Wilaya ya Kahama Annamringi Macha amepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe na usafirishaji wa nguruwe wenyewe baada ya wanyama hao kubainika kuwa na homa ya nguruwe.
Akizungumza na waandishi wa habari, DC Macha amesema amechukua uamuzi huo ili kukinga wananchi na watumiaji wa nyama hiyo dhidi ya ugonjwa huo.
‘’Maeneo yanayofanya biashara ya nyama ya nguruwe, vichinjio, wapishi na sehemu za starehe haziruhusiwi kufanya biashara hiyo kwa sasa mpaka itakapotangazwa tena,’’ Macha
Macha amesema dalili za mlipuko wa ugonjwa huo zilianza Desemba mwaka jana na sasa ni kama unasambaa.
Macha pia alipiga marufuku usafirishaji wa wanyama hao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali cha daktari na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.
Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dkt. Damian Kilyenyi amethibitisha kuwa zaidi ya nguruwe 500 wamekufa kwasababu ya ugonjwa huo.
0 Comments