TANGAZA NASI

header ads

Kocha Yanga: Simba awakupaswa kumsajili Chikwende



 MOHAMED Hussein, mmachinga, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Princess amesema kuwa anaamini kwamba wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba hawakupaswa kumsajili winga, Perfect Chikwende raia wa Zimbabwe kwa kuwa wanawachezaji wengi kwenye idara hiyo.

Simba ambayo kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola imekamilisha usajili wa Chikwende kwa dili la miaka miwili huku ikielezwa kuwa dau lake ni milioni 127 la usajili wake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa kwa namna mahitaji ya kikosi cha Simba yalivyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu Bara haikuwa na sababu ya kumvuta winga kwenye kikosi.

"Ninavyoona mimi kwa Simba kumsajili Chikwende ni maamuzi mazuri ila hayana faida hasa kwenye uhitaji na makosa ambayo yanaonekana ndani ya wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Inaonekana mbele ina safu kali ya ushambuliaji na kwa upande wa mawinga inao wengi wenye uwezo mkubwa ambao wanafunga na kutengeneza nafasi za kufunga hivyo itakuwa ngumu kwake kuweza kujenga ufalme mpya.

"Inahitaji kumpata beki mzuri wa kati ambaye atakuwa akituliza mashambulizi huku kwenye safu ya kiungo mkabaji pia ikiongeza nguvu ila kumleta winga kwa sasa naona bado ni maamuzi ambayo hayakupaswa kufanyika kwa sasa.

"Yote kwa yote ni mchezaji mzuri na usajili wao ni suala la kusubiri namna gani mambo yatakuwa kwenye mechi ambazo atacheza ila asifikirie kuwa mfalme kwa wakati huu," 

Post a Comment

0 Comments