Na John Walter- Babati
Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kimeiomba serikali na wadau wa mchezo wa Netiboli kusaidia mahitaji muhimu yatakayoweza kufanikisha mashindano ya kitaifa yalioanza januari 3,2021 mkoani Manyara.
Wametoa ombi hilo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Netiboli (TAIFACUP2021) ambayo yameanza kutimua vumbi katika viwanja vya Kwaraa na Shule ya Sekondari Singe mjini Babati.
Katika risala ya Chama cha Netiboli (CHANETA) iliyosomwa na Hilda Mwakatobe Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania, ilieleza kuwa timu zilizofika zinakabiliwa na upungufu wa Chakula, malazi ukosefu wa usafiri kwa viongozi na waamuzi ambapo upungufu huo ni zaidi ya shilingi milioni tano.
Risala hiyo ileleza kuwa mashindano hayo yalipangwa kushirikisha timu 26 za Tanzania Bara lakini kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao zilizofika hadi sasa ni 10 tu.
Mikoa iliyofika kushiriki ni mwenyeji Manyara,Mbeya, Simiyu, Tabora, Arusha, Zanzibar, Mara.
Mkurugenzi Msaidizi anaeshughulikia maendeleo ya michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Adolf Kopa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari utamaduni, Sanaa na Michezo Inncocent Bashungwa , amesema atawasilisha kwa waziri risala na changamoto zilizowasilishwa na kutolewa majibu.
Amewapongeza Viongozi wa mkoa wa Manyara na CHANETA kwa ushiriki na ukaribu waliounyesha katika kuandaa na kuendesha mashindano hayo yaliyoshirikisha mikoa mbalimbali kutoka Bara na Visiwani.
Katika risala ya Chama cha Netiboli (CHANETA) iliyosomwa na Hilda Mwakatobe Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania, ilieleza kuwa timu zilizofika zinakabiliwa na upungufu wa Chakula, malazi ukosefu wa usafiri kwa viongozi na waamuzi ambapo upungufu huo ni zaidi ya shilingi milioni tano.
Risala hiyo ileleza kuwa mashindano hayo yalipangwa kushirikisha timu 26 za Tanzania Bara lakini kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao zilizofika hadi sasa ni 10 tu.
Mikoa iliyofika kushiriki ni mwenyeji Manyara,Mbeya, Simiyu, Tabora, Arusha, Zanzibar, Mara,Dodoma,Mwanza, Dar es Salaam.
Lengo la mashindano hayo ni kuendeleza mchezo wa netiboli na kuweza kuchagua wachezajii wa timu ya taifa itakayowakilisha nchi katika mashinadano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi na kutoa hamasa kwa wananchi kuupenda mchezo huo.
Mashindano hayo ya ligi kuu ya Taifa ni mashindano ya nne tangu uongozi uingie madarakani mwaka 2017
0 Comments