Iran imeamua kulipa fidia ya dola 150,000 kwa familia za kila mtu aliyepoteza maisha katika ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Ukraine, ambayo iliangushwa na kombora kwa bahati mbaya mnamo Januari.
Fidia inayolipwa kwa familia za wale waliopoteza maisha kwenye ndege ya abiria ya Shirika la ndege la Ukraine iliidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Baraza la Mawaziri liliidhinisha malipo ya dola 150,0000 kwa familia na jamaa za kila mmoja ya wale waliokufa kwenye ndege ya Ukraine haraka iwezekanavyo.
Ndege ya abiria ya aina ya "Boeing 737" ya Ukraine iliangushwa muda mfupi baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran kwenda Kiev asubuhi ya Januari 8, ambapo hakuna abiria yeyote kati ya watu 176 aliyeweza kunusurika.
Hapo awali, maafisa wa Iran walikuwa wakikanusha madai ya kuilenga ndege hiyo na baadaye Idara ya Ulinzi ikatangaza kwamba ndege hiyo ya Ukraine ilipigwa kombora kwa bahati mbaya baada ya makombora mawili yaliyorushwa na mfumo.
Masaa machache kabla ya kuangushwa kwa ndege hiyo, Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Iran lilifanya shambulizi la kombora kwenye kambi za Marekani zilizoko nchini Iraq kulipiza kisasi cha mauaji ya jenerali wa Iran Qassem Soleimani.
0 Comments