Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amepata nafasi ya hifadhi ya kisiasa nchini Canada.
Taarifa kutoka nchini Kenya zinasema, Lema ameondoka jana nchini humo akiwa na familia yake, Wakili wake George Luchiri Wajackoyah amethibitisha.
Mwezi uliopita Polisi nchini Kenya walimkamata kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria na kumuachia huru baada ya muda mfupi.
Kwa mujibu wa Wakili wake, Wajackoyah, Lema ambaye alikua ameambatana na familia yake alikua akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kutishiwa maisha.
0 Comments