Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amemualika mpinzani wake, Rais wa zamani Henri Konan Bédié kwa ajili ya mazungumzo baada ya kutokea vurugu zilizosababishwa na ushindi wake wa kishindo kuelekea kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu.
Viongozi wa upinzani walisusia kura za mwezi uliopita na kuapa kuunda serikali ya mpito ambayo itaandaa uchaguzi mpya.
Siku ya Jumatatu mahakama ya kikatiba ilithibitisha ushindi wa Bw.Ouattara.
Alipata 94.27% ya kura zilizopigwa. Hakuna rufaa dhidi ya uchaguzi wa rais unaowezekana sasa, kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo.
Rais Outtara alimualika Bw. Bédié kwenye ‘’mkutano siku chache zijazo kwa ajili ya mazungumzo ya wazi na ya kweli kusaidia kurudishauaminifu,’’ Shirika la habari la Ufaransa limeripoti.
Viongozi kadhaa wa upinzani wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi na uchochezi baada ya kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ouattara.
Takribani watu 40 wameuawa kutokana na vurugu zinazohusiana na uchaguzi tangu mwezi Agosti.
0 Comments