MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema Serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo haitosita kutumia mbinu mbadala ya ulinzi wa mbwa na farasi katika kukabiliana na kuwadhibiti wale wote watakaonekana kutaka kuvuruga amani ya nchi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
Jokate amesema hayo akiwa katika Chuo cha Polisi cha mafunzo ya Mbwa na Farasi kilichopo Zegelo wilayani Kisarawe ametumia nafasi hiyo kufafanua pia mbwa na farasi hao watatumika kukabiliana na mapigano ya mara kwa mara kati wakulima na wafugaji.
Akizungumza baada ya kutembelea chuo hicho cha mafunzo ya mbwa na farasi kinachosimamiwa na jeshi la polisi ikiwa ni ziara yake ya kujionea namna wanyama hao wanavyoweza kutumika katika kukabiliana na matukio ya uhalifu Jokate amesema nia ya Serikali ni kuona taifa linakua na utulivu wakati woe.
Hivyo Serikali inatumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kutumia mbwa na farasi katika kukabiliana na matukio ua uhalifu na wahalifu huku akitumia nafasi hiyo kuzitaka jamii za wakulima na wafugaji kujiepusha na migogoro ambayo imekua ikihatarisha uvunjifu wa amani kila uchwao ndani ya Wilaya yao ya Kisarawe.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo ya mbwa na farasi kutoka Jeshi la Polisi Kyariga Majura ametoa ushauri kwa jamii kuhakikisha wanapeleka mbwa wao chuoni hapo ili wapatiwe mafunzo yatakayosaidia kuimarisha ulinzi wa mali zao.
0 Comments