TANGAZA NASI

header ads

Wanahabari Lindi, Pwani, Ruvuma na Mtwara wanolewa na kuaswa waandike habari sahihi.



Na Ahmad Mmow, Lindi. 


Waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani wameaswa waandike kwa usahihi habari  zinazohusu mpango  wa kunusuru masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF) ili jamii ipata taarifa za kweli zinazohusu mpango huo.


Wito huo umetolewa leo mjini Lindi na Katibu tawala wa mkoa( RAS) wa Lindi, Rehema Madenge wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uelewa waandishi wa habari hao  kuhusu mzunguko wa pili wa awamu ya tatu ya utekelezaji wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini.


Madenge alisema wanahabari ni nguzo muhimu ya kuelimisha , kufundisha na kuhabarisha jamii taarifa mbalimbali, tena za kweli na sahihi.


Alisema watu wengi wanasikia mpango huo na wataka kujua ukweli wa hayo wanayosikia. Kwahiyo waandishi wa habari ambao wanafika katika maeneo ya utekelezaji wanakila sababu ya kueileza jamii kuhusu ukweli na usahihi wa wanayo yaona.


RAS huyo wa mkoa wa Lindi alisema kazi ya uandishi ni ibada. Hasa wasndishi wanapo andika habari chanya zinazogusa watu wengi na hatimae watu hao wakabadilika kutoka katika hali moja na kwenda hali nyingine ya mafanikio.


Madenge aliwaasa pia waandishi hao kutumia mafunzo hayo kama darasa la kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu mpango huo. Kwahiyo waulize na kujifunza Mambo ambayo walikuwa hawayajui ili wawe mabalozi kwa jamii.


Alibainisha kwamba  vyombo vya habari vina nguvu kubwa, vinaaminiwa na vinaushashi mkubwa kwa jamii. Hivyo waandishi watumie sifa hizo kuelimisha jamii na kuandika habari za kweli na sahihi. Kwani wanao uwezo  wakufuta upotoshaji na kueleza ukweli na usahihi wa jambo husika.


Kwaupande wake mkurugenzi mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga alisema   nia ya kikao kazi hicho nikuwajengea uelewa waandishi hao ili ujumbe uwafike wadau na walengwa kupitia kalamu zao.


Alisema licha ya kikao kazi lakini pia watakwenda kwa walengwa ili kuona utekelezaji wa mpango. Lengo likiwa ni waandishi hao wapate na watoe mrejesho sahihi wa yale watakayo yaona na kujifunza.


 Kwaupande wake mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi( LRPC), Christopher Lilai licha ya kuishukuru TASAF kwa kuandaa kikao kazi hicho lakini pia alipongeza mfuko huo kwakuthamini na kutambua umuhimu wa vyombo vya habari.


Alisema TASAF  imekuwa ikiandaa mafunzo, semina na vikao kazi na waandishi wa habari mara nyingi. Hali inayoonesha kwamba mfuko huo umewaweka waandishi wa habari kama sehemu ya mfuko huo na mafanikio yake.



Post a Comment

0 Comments