Jumuiya ya Ulaya (EU), imetangaza kujumuisha mawaziri wengine 7 wapya wa serikali ya Bashar Assad nchini Syria, kwenye orodha ya watu watakaowekewa vikwazo.
Kulingana na taarifa za baraza la EU, iliarifiwa kuwa idadi ya watu waliokuwa vikwazo imefikia 280 ikiwa ni pamoja na watu wa serikali ya Assad.
Orodha hiyo pia inaarifiwa kujumuisha mashirika 70.
Vikwazo hivyo vilivyowekwa vinahusu marufuku ya usafiri na uzuiaji wa milki za wahusika.
EU ilichukuwa hatua ya kuweka vizuizi dhidi ya serikali ya Syria tangu mwaka 2011 ambavyo ni marufuku ya uagizaji wa mafuta, vikwazo vya baadhi ya uwekezaji, kufungia mali za Benki Kuu ya Syria zilizowekwa katika EU, kizuizi cha usafirishaji wa vifaa na teknolojia inayotumika kushinikiza umma na kuzuia mawasiliano.
0 Comments