TANGAZA NASI

header ads

JOWUTA yawapiga msasa waandishi wa habari Njombe



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia  usalama ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea katika majukumu yao ya kila siku.

Wito huo umetolewa na wakufunzi kutoka Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) wakati wakitoa semina kwa wanahabari katika ukumbi wa Dosmeza mjini Njombe juu ya maswala ya Jinsia na usalama mahala pa kazi.



Sophia Ngalapi ambaye ni mkufunzi kutoka Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) akitoa mafunzo ya jinsia na namna wanahabari wanavyotakiwa kufanya habari zinazohusu jinsia.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika majadiliano ya kundi mara baada ya mafunzo yaliyokuwa yakiendelea mjini Njombe



Emilia Msafiri  Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Radio King's akiwa ameshika tunda aina ya Tufaha (Apple) na Judica Schone mwanahabari akiwa ameshika tunda aina ya Chungwa wakati wa kuonyesha usawa na utofauti wa matunda hayo kwa dhana ya kujenga umoja na mshikamano kwa wanahabari.


Wanahabari wakiwa katika kundi la pamoja ili kujadili moja ya mada waliyopewa na mkufunzi wakati wa mafunzo.


Post a Comment

0 Comments