Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kanisa la Romani Katoliki
parokia ya Utalingolo jimbo la Njombe mbioni kupata gari ya usafiri kwa ajili
ya parokia kutokana na kukusanya Shilingi milioni hamsini na nne,laki tisa na
arobaini na moja elfu,na mia nne hamsini (54,941,450/=) kutoka kwa wadau mbali
mbali na harambee iliyofanyika mapema
August 2/2020 katika kanisa hilo.
Awali akitoa taarifa ya
Parokia kwa niaba ya kamati ya harambee ya ukusanyaji wa fedha za ununuzi wa
gari Ndug,Deo Mtewele amesema Parokia yenye vigango vinne vya
Utalingolo,Igoma,Iliwa na Luhuji ilianzishwa rasmi mwaka 2011,lakini kumekuwa
na shida ya utoaji wa huduma kutokana na kukosa usafiri huku ikilazimu kutumia
njia mbali mbali ikiwemo kuazima kwa wadau
“Licha ya Changamoto
ya usafiri lakini Parokia yetu imefanikiwa kufanya shughuli mbali mbali za
kitume,pamoja na mafanikio moja ya changamoto yetu ni ukosefu wa gari ya
Parokia kama chombo cha kurahisisha huduma mbali mbali za Kichungaji”alisema
Deo Mtewele
Daktari Tobias
Lingalangala ni mgeni wa heshima katika harambee ya ununuzi wa gari ilyofanyika
katika kanisa hilo,kutokana na kuona changamoto za kanisa ameweza kuchangia
shilingi Milioni 15 na kulitaka kanisa kutafuta gari mapema inayoweza kuendana
na fedha iliyopatikana kuliko kusubiri kutafuta Milioni 100 ya makadilio na
mahitaji yalio kuwa yamepangwa na kamati.
“Mtafute gari ambayo
itakuwa nzuri na kwa hizi fedha mlizokusanya mkishirikiana na mimi kwa utulivu
na kwa kuamini tunaweza kununua gari nzuri sana,kwa fedha hizi inawezekana” Alisema Dkt,Thobias
Lingalangala Mgeni wa
heshima harambee ya ununuzi wa gari ya Parokia ya Utalingolo,jimbo la Njombe.
Mwenyekiti wa kamati ya harambee Ndugu,Erasto Mpete amesema
hawakuweza kutajia kupata kiasi hicho cha fedha kwa kuwa sio kitu kidogo kwao.
“Tukiongeza na kitita cha Mgeni rasmi kwenye fedha
tulizokusanya jumla yake inatufanya kuwa na jumla ya milioni hamsini na nne
laki tisa na arobaini na moja mia nne hamsini,kwa maneno mengine wanaparokia ya
Utalingolo tumechanganyikiwa,kwa kweli tunamshukuru sana mgeni rasmi”alisema
Erasto Mpete
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesema hatua waliyofikia
ni jambo la kushukuru Mungu kwa kuwa wanaamini Parokia yao sasa kupata usafiri
kwa ajili ya Paroko utakaomuwezesha kufika sehemu yoyote kwa wakati.


0 Comments