Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Malawi imetupilia kapuni ombi la Kenya Airways kuanza safari nchini humo ikisema kuwa inaendelea kuchukua hatua za tahadhari kabla ya kufungua anga yake.
Hii inafuatia tangazo la Kenya Airways kuanza safari Agosti 1 katika baadhi ya nchi ikiwa ni baada ya kusitisha safari zake kwa muda mrefu kufuatia mlipuko wa Covid-19. Katika barua hiyo James Chakwera ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga amesema kwamba Idara ya anga baada ya kushauriana na mamlaka nyingine imeamua kuendelea kuifunga anga ya nchi hiyo kwa muda.
Mapema jana Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilitangaza kuisitisha kwa muda Kenya Airways kutua katika viwanja nchini ikiwa ni hatua baada ya Kenya kuiondoa Tanzania katika orodha ya nchi ambazo raia wake wanaruhusiwa kuingia.


0 Comments