Na
Amiri Kilagalila,Njombe
Wanafunzi
wa Kidato cha tano katika shule ya sekondari Lupila iliyopo wilayani Makete
mkoani Njombe,wametakiwa kufuata na kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa
katika shule hiyo ikwemo kuepuka migomo ili waweze kufanikiwa kupata elimu bora
itakayowasaidia katika maisha yao.
Hayo
yamebainishwa mwishoni mwa wiki katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi hao
wa kidato cha 5 katika shule hiyo ambapo mgeni rasmi Kaimu Mtendaji wa kata ya
Lupila Esau Pagalo amesema wanafunzi hao wanatakiwa kuzingatia masomo na
wajiepushe na migomo.
“Muwe
tayari kusoma katika shule yetu hii ya Lupila,mnapofika hapa fateni na
kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa hapa shuleni,walimu wapo tayari kuwa
na ninyi na hatutegemei kabisa kutokea migomo”alisema Esau Pagalo
Mkuu
wa shule hiyo Mwl Abokasa Ngwale amesema walimu wa shule hiyo wamejipanga
kuwafundisha ipasavyo wanafunzi hao huku serikali ikiwa imewapangia wanafunzi 75 kwa
maana kila mkondo wanafunzi 25, ambapo mpaka sasa wameripoti wanafunzi 50
“Serikali
ilitupangia wanafunzi 75 kwa EGM wanafunzi 25,HGK wanafunzi 25 na HKL wanafunzi
25 na kufanya jumla jumla 75 ingawa kama shule tuliomba wanafunzi 40 sasa
tumeongezewa na hiyo sio changamoto kwetu” alisema Abokasa Ngwale
Naye
Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi shuleni hapo Bw. Nuhu Sanga amesema michango ya
wananchi inawasaidia kuendelea na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa
ambavyo Wanatarajia kuvitumia kama mabweni
“Hali
ya ujenzi wa maeneo ya shule yanaenda vizuri japo sio sana kwasababu kuna mambo
mengine bado hatujakamilisha,tunategemea michango kutoka kwa wananchi ili
tuendelee kukarabati vyumba viwili vya kulala wanafunzi “alisema Nuhu Sanga
Shule
ya sekondari Lupila wilayani Makete mkoani Njombe ni miongoni mwa shule zilizopewa kibali na
kuanzisha kidato cha tano na sita mwaka huu 2020.
0 Comments