Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imelaani taarifa za maafisa wakuu wa Ugiriki na maandamano yaliofanywa nchini humo baada ya waislamu kufanya sala katika jengo maarufu la Haggia Sophia.
Wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya kudumishwa kwa demokrasia nchini Ugiriki, waziri mkuu wa nchi hiyo Kyriakos Mitsotakis aliitaja hatua ya Uturuki ya kulibadi jengo hilo kuwa uchokozi na fedheha kwa ustaarabu katika karne hii ya 21.
Lawama za Ugiriki kuhusu kugeuzwa kwa jengo la Hagia Sophia na kuwa msikiti baada ya jengo hilo kutumika kwa miongo kadhaa kama makavazi, zimezusha mvutano kati ya Ugiriki na Uturuki.
0 Comments